Kitengo hiki cha tuzo hutuzwa watu binafsi au mashirika ambayo kazi zao kuu huimarisha maarifa na teknolojia ya binadamu, na kuathiri mazingira kwa njia chanya.
Washindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia huchaguliwa na jopo la kimataifa kufuatia mchakato wa upendekezaji unaofanywa na umma. Idadi kubwa ya wanaopendekezwa inaonyesha jinsi ambavyo idadi ya watu wanaelewa kinachowezekana na kuona fursa katika kutunza na kuboresha mazingira inavyoongezeka.
Mabingwa wa Dunia ni sehemu ya watu ambao matendo yao mema yamepelekea ushindi wa mazingira ambao umebadilisha jamii zetu kuwa bora. Kukomeshwa kwa matumizi ya kemikali zinazoharibu ozoni, kuondolewa kwa risasi kwenye petroli, kupiga marufuku matumizi ya plastiki inayotumika mara moja moja, utunzaji wa viumbe walio hatarni kuangamia na kuongezeka kwa matumizi ya nishati jadidifu ni kunatokana na kujitolea kwa watu, bidii yao, ushirikiano wao na uvumbuzi wao.